Ili kufanikiwa lazima kufanya juhudi na kujituma. Hii imemtokea James Msuva baada ya kufanya majaribio na kufuzu kuichezea Mbao FC.
James ni mdogo wake winga wa Yanga, Simon Msuva ambaye sasa ni kati ya wachezaji nyota nchini kutokana na juhudi zake.
James
aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga U20 na msimu uliopita wa Ligi Kuu
Bara alikuwa akiichezea JKT Ruvu, alitua kwenye majaribio hayo wiki
iliyopita kabla ya kupewa majibu hayo ya kufuzu.
Mbao
hivi sasa ipo kwenye mikakati ya kukisuka upya kikosi chake
kilichoondokewa na karibu nusu ya wachezaji mahiri waliotua Simba,
Yanga, Azam FC na kwingineko.
Akizungumza na Championi Jumatano, James alisema anafurahi kuwa mmoja wa wachezaji watakaoichezea Mbao msimu ujao wa ligi kuu.
Alisema
baada ya kupata majibu hayo, hivi sasa anasubiria kusaini mkataba
atakaopewa wakati wowote kuanzia hivi sasa baada ya kufikia makubaliano
mazuri.
“Ninafurahi
kuwemo kati ya wachezaji watakaounda kikosi cha Mbao, hiyo ni baada ya
kufuzu majaribio haya ya wiki, hivyo muda wowote ninatarajiwa kusaini
mkataba,” alisema James anayemudu kucheza namba 7, 9, 10 na 11.
Kwa
upande wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mrundi, Etienne Ndayiragije,
alithibitisha kufuzu kwa James: “Nina wachezaji wengi waliojitokeza
kwenye majaribio ya timu yangu na James ni miongoni mwa wachezaji hao
ambaye yeye amefuzu.”
Katika
majaribio hayo tofauti na James alikuwepo Amos Abel, aliyewahi
kuichezea timu ya vijana ya Yanga na kipa Kabali Faraji, aliyewahi
kuzichezea Simba na African Sports iliyoshuka daraja.
No comments:
Write comments