Simba imemsajili Mbonde kwa mkataba wa miaka miwili, hivyo kuongeza idadi ya mabeki wakiwemo Shomari Kapombe aliyesajiliwa kutoka Azam FC, Ally Shomari (Mtibwa) na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ aliyepo kikosini.
Simba inaweza kuwajaribu mabeki hao Agosti 23, mwaka huu katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkude amesema ujio wa Mbonde katika kikosi chao umeleta chachu kwa kuwa na mabeki imara ambao wanaifanya timu kubwa bora kupambana na timu yoyote hata Yanga.
“Ujio wa Mbonde Simba umeongeza ushindani katika safu yetu ya ulinzi pia inakifanya kikosi chetu kiweze kuwa imara zaidi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu, Yanga wajiandae.
“Tutakutana nao kwanza katika mechi ya Ngao ya Jamii, tupo vizuri na kwa safu yetu hii ya ulinzi naamini Yanga watapata tabu kutupita tofauti na huko nyuma,” alisema Mkude.
No comments:
Write comments