Monday 17 July 2017

KESI YA JAMALI MALINZI KIZUNGUMKUTI




Kesi inayowakabili Rais wa TFF, Jamal Malinzi, Katibu TFF, Mwesigwa Celestine na mhasibu wa shirikisho hilo, imeahirishwa hadi Julai 30.

Malinzi na wenzake wanaotuhumiwa katika makosa zaidi ya 25 yakiwemo ya matumizi mabaya ya ofisi pia utakatishaji fedha, walifikishwa tena leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kabla ya kuahirishwa.

Moja ya makosa yanayowakabiri ni utakatishaji fedha ambalo halina dhamana. Watuhumiwa hao wamerejeshwa mahabusu tena

No comments:
Write comments