Aliyekuwa Msema wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Klabu ya
Yanga, Jerry Muro ameiponda Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kwa kusema kuwa kamati hiyo ina mapungufu makubwa.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kamwe uonevu
kama huo wanaoufanya kamati ya maadili ya TFF utaendelea kudidimiza
mchezo mpira wa miguu hapa nchini.
“Nadhani mmeona kilichotokea kwa baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu
wa shirikisho hilo kule walipo sasa hivi, walijua hawatajulikana ubaya
ambao waikuwa wakiufanya, wakasahau kuwa siku itafika na
wataumbuka,”amesema Muro.
Aidha, amesema kuwa Kamati hiyo haikutumia hekima kuweza kutoa
maamuzi yaliyopelekea kufungiwa huku akiongeza kuwa mchezo wa mpira wa
miguu sasa hivi unahitaji watu wenye uelewa na mchezo huo ili uweze
kufika mbali zaidi.
Hata hivyo, Jerry ameushukuru uongozi wa Klabu yake ya Yanga kwa
kufanya nae kazi vizuri mpaka pale mkataba wake uipomalizika,pia
ameipongeza Klabu hiyo kwa kupata msemaji mpya.
Tuesday, 18 July 2017
VIDEO:JERRY MURO ATEMA CHECHE,ARUSHA KOMBORA KWA KAMATI YA MAADILI YA TFF
KAMA ULIKOSA KUMTAZAMA HARMORAPA AKITINGA MSIBANI KWA WAZIRI MWAKIEMBE BONYEZA HAPA CHINI UJIONEE MWENYEWE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments