Monday 21 August 2017

JOTO LA NGAO YA HISANI LAONGEZEKA TFF YASOGEZA MUDA WA MECHI HIYO YA WATANI WA JADI




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema mechi ya watani Yanga na Simba, itaanza saa 11 jioni.

Awali mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, ilipangwa kuanza saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, keshokutwa Jumatano.


Lakini Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ametangaza mabadiliko hayo ya ratiba ya mchezo huo kusogezwa kwa saa moja zaidi.

No comments:
Write comments