Saturday 26 August 2017

MANARA MDOMO WAMPONZA MASAU BWIRE,SIMBA WAWAUNGIA WANAJESHI KIFURUSHI CHA WIKI

Image result for okwi

Msemaji wa Simba Haji Manara amesema kilichowaponza Ruvu ni maneno machafu ya Masau na kwakichapo hicho timu yake ilichopokea ataenda kufunzwa kuongea na waajiri wake.
napia anauhakika kwa ushindi huo mkubwa Simba itakua kileleni kwani hakuna timu itakayofunga idadi hiyo ya magoli au zaidi ktk michezo ya ufunguzi hii leo,pia hakusita kuwakosoa waliomwita Okwi babu na kusema shughuli yake wameiona
FULL TIME
Dk ya 92: Mchezo umemalizika, Simba wamepata ushindi mnono wa mabao 7-0.
Dk ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.
Dk ya 89: Kiungo wa Simba Kotei anachezewa faulo, amchezo unasimama kwa muda.
Dk ya 85: Simba wanaongoza kwa mabao saba hadi sasa, Ruvu wanatumia muda mwingi kulaumiana.
Simba wanapata bao la saba kutpia kwa Erasto Nyoni.
Dk ya 82: GOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 80: Wachezaji wa Simba sasa wanaonyesha ufundi uwanjani.
Dk ya 75: Mchezo ni wa kushambuliana kwa zamu.
Dk ya 70: Kasi ya Juuko bado haijachanganya.
Dk ya 65: Simba wanafanya mabadiliko, wanamtoa Mwanjali, anaingia Juuko. 
Dk ya 61: Kichuya anapata nafasi ya kufunga lakini anakuwa ameotea. 
Dk ya 57; Mchezo unaendelea kwa kasi, Simba ni kama hawajatosheka na mabao waliyofunga.
Dk ya 51: Okwi anaipatia Simba bao la Sita, anafunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Saidi Ndemla ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Niyonzima aliyeumia.
Dk ya 51: GOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 50: Ruvu wanasogea kwenye lango la Ruvu lakini wanazuiwa.
Dk ya 48: Simba wanacheza mchezo wa nguvu, Kotei anacheza faulo katikati ya uwanja.Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.
Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO
Dk ya 47: Mwamuzi anamaliza kipindi cha kwanza Simba wakiwa mbele kwa mabao 5-0.
Simba wanapata bao la tano likifungwa na Juma Liuzio akimalizia krosi nzuri ya Nyoni.
Dk ya 46: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.
Simba wanapata bao la nne kupitia kwa Kichuya, alipata krosi nzuri kutoka kwa Nyoni akamalizia kiulaini.
Dk ya 42: GOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 40: Mashabiki wa Simba wanashangilia kwa nguvu hapa kwenye Uwanja wa Uhuru.
Dk ya 38: Simba wamemiliki mchezo kwa muda mrefu sasa.
Pasi nzuri kutoka kwa Mzamiru, inatua mguuni kwa Okwi, akiwa yeye na kipa anatupia bao la tatu.
Okwi tenaaaaaaaaa
Dk ya 35: GOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!
Dk ya 32 Mchezo unaendelea, Manula ameshatibiwa.
Dk ya 30: Mchezo umesimama, kipa wa Simba, Aishi Manula amelala chini baada ya kuumia.
Dk ya 25: Simba wanamiliki mpira muda mwingi, mashabiki wao wanashangilia kwa nguvu.
Okwi tena anaipatia bao la pili Simba, amewapiga chenga mabeki wawili na kutupia mpira wavuni.
Dk ya 22: Gooooooooooooooooooooo!
Dk ya 20: Simba wanaongoza bao 1-0.
Okwi anaipatia Simba bao la kwanza baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Ruvu kisha kupiga shuti lililojaa wavuni moja kwa moja, alipata pasi kutoka kwa Mzamiru.
Dk ya 18: Okwiiiiiiiiiiiiiiii
GOOOOOOOOOOOOOOOOO!!
Dk ya 16: Ruvu wanacheza vizuri kadiri muda unavyokwenda, wanapa upinzani Simba.
Dk ya 14: Mzamiru anacheza faulo katikati ya uwanja, unapigwa mpira kuelekea kwa Simba.
Dk ya 10: Simba ndiyo ambao wamefila langoni mwa Ruvu lakini hawajaweza kutengeneza mashambulizi ya nguvu.
Dk ya 6: Simba wanalishambulia lango la Ruvu lakini bado kasi haijachanganya.Dakika ya 1: Timu zote zimeanza kwa kasi ndogo.
Mchezo umeanza.
Timu zimeshaingia uwanjani.

SIMBA SC 
1. Aishi Manula-28
2. Ally Shomary-21
3. Erasto Nyoni-18
4. Method Mwanjale-17
5. Salum Mbonde-2
6. James Kotei-3
7. Shiza Kichuya-25
8. Mzamiru Yassin-19
9. Juma Liuzio-10
10. Emmanuel Okwi-7
11. Haruna Niyonzima-8

SUB
1. Emmanuel Mseja-30
2. Jonas Mkudeh-20
3. Mohamed Ibrahim-4
4. Said Ndemla-13
5. Laudit Mavugo-11
6. Juuko Murshid-6
7. Mohamed Hussein-15

Kocha... 
MARIUS OMOG

RUVU SHOOTING. 

1. Bidii Hussein-18
2. Said Imani Madega-19
3. Yusuph Innocent-2
4. Shaibu Nayopa-26
5. Mangasin Mangasin-6
6. Baraka Mtuwi-15
7. Chande Magoja-21
8. Shaban Msaja-4
9. Juma Said-9
10. Jamal Mtegeta-10
11. Khamis Mussa-22

Subs. 

1. Abdallah Rashid-1
2. George Wawa-12
3. Mau Ally-23
4. Frank Msese-16
5. Kassim Dabi-24
6. William Patrick-27
7. Said Dilunga-25

Kocha.. 
ABDUL MUTIK HAJI

Kick Off-16:00

No comments:
Write comments