Yanga imethibitisha itawakosa wachezaji wake watatu katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba kesho Jumatano.
Mchezaji wa kwanza ni ni Obrey Chirwa ambaye anasumbuliwa na kifundo cha mguu na Geofrey Mwashiuya anayesumbuliwa na goti.
Pamoja na hao mawinga au viungo wa pembeni, Yanga itamkosa kipa wake Beno Kakolanya ambaye pia anasumbuliwa na bega.
Msemaji wa Yanga, Disman Ten amesema, ukiachana na wachezaji hao wengine wote wako fiti kabisa.
“Wengine wako katika hali nzuri kabisa na kilichobaki ni suala la mwalimu mwenyewe atasema anamtumia nani,” alisema.
No comments:
Write comments