Tuesday, 22 August 2017

UMEMSIKIA MASAU BWIRE ALICHOSEMA KUELEKEA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA KESHO


Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema watu hawana raha mitaani kwa kuwa gumzo pekee ni Yanga na Simba kwa kuwa zinakutana kesho.

Lakini akasisitiza, timu hizo hazina lolote kwa kuwa zina mambo ya kitoto kwa kuwa huwa hazionyeshi soka lolote zaidi gumzo la mazoea.

Yanga na Simba zinakutana kesho kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya Ngao ya Jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Masau ambaye ni mwalimu kitaaluma, amesema hakuna kipya ambacho timu hizo huwa zinaonyesha.

“Nikuambie hawa jamaa hawana lolote hasa kama unazungumzia uwanjani. Mimi naona ni mambo ya kitoto tu, gumzo kubwa kila sehemu mtaani hadi hatuna raha.


“Lakini ukienda uwanjani pale, hakuna kiwango chochote kinachoonyeshwa,” alisema.

No comments:
Write comments