Advertisement

Saturday, 7 April 2018

SIMBA KUMRUDISHA CHIRWA BONGO

Image result for chirwa picha

Jumatano wiki hii straika wa Yanga, Obrey Chirwa alienda kwao Zambia kutokana na matatizo ya kifamilia, sasa uongozi wa klabu hiyo umesema mchezaji huyo anarudi muda wowote kuanzia sasa kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.

Chirwa hatacheza mechi ya leo ya Yanga dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwani ana kadi mbili za njano, hivyo kwa mujibu wa kanuni hatocheza.

Chirwa alipata kadi hizo katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers ya Boswana.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa, Chirwa atarejea baada ya wiki moja ili kuwahi maandalizi ya mechi dhidi ya Simba itakayochezwa Aprili 29, mwaka huu.

“Chirwa aliondoka kwa ruhusa ya wiki moja kwenda nyumbani kwao kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia, hatutarajii akae sana huko kwa kuwa anatakiwa awahi kurudi kwa ajili ya maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Simba,” alisema Ten. 

Chirwa ana mabao 12 kwenye Ligi Kuu Bara, na amekuwa msaada mkubwa kwa Yanga kutokana na uhodari wake wa kuzifumania nyavu.

Sunday, 25 March 2018

ISHU YA WAMBURA IMEFIKA PATAMU,MANARA AJICHENGA KIMTINDO

Image result for HAJI MANARA FT MICHAEL WAMBURA

Kazi mpya imeibuka baada ya aliyekuwa Makamu Rais wa TFF, Michael Wambura kumtumia Msemaji wa Simba, Haji Manara katika moja ya picha zinazosambaa kama kauli yake.

Kauli hiyo inaeleza makosa kadhaa ya Rais wa TFF, Wallace Karia kama kuruhusu mambo kuendeshwa kienyeji ikiwa ni pamoja na waliokuwa wanatumikia adhabu kuruhusiwa kufuata utaratibu uliowaondolea adhabu kinyume cha katiba ya TFF.

Wambura amemtaja Manara na Dk Damas Ndumbaro, jambo ambalo limemfanya Manara naye kujibu mapigo akimtaka Wambura amalizane na TFF na si yeye, huku akisisitiza “anaujua mziki wake”.

“Michael Wambura usinichokoze na usitafute huruma kupitia migongo ya watu,” anaandika Manara.

Anaendele: “Wala usimzushie Rais katika shauri langu na TFF, mimi sio maji yako nadhani unanijua vizuri. …Vita hii hainihusu ila unalazimisha kununua ugomvi, nikufahamishe tu kuwa shauri langu sikukuta rufaa, niliomba review sababu sikupewa nafasi ya kusikilizwa na huyo wakili wako (Emmanuel Muga), ndiye alishiriki kunihukumu bila kusikilizwa leo mnapata wapi moral authority ya kulalamika?”

“Watu mlioshiriki kutuonea wenzenu!! Nakuweka kiporo ukiendelea utachokoza jeshi la mtu mmoja litakaloeleza mengi yaliyojificha nyuma ya pazia.”


Wambura amefungiwa kujihusisha na soka maisha ikiwa ni baada ya kupatikana na hatia ya kugushi baadhi ya nyaraka na kuchukua fedha zilizoelezwa ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo Wambura amekata rufaa kupinga mchakato mzima uliotumika kumfungia.

Lakini tayari Kamati ya Utendaji ya TFF, imemteua Athumani Nyamlani kukaimu nafasi ya Wambura.

POGBA,SHAW WAMUWEKA MOURINHO KUTI KAVU


Image result for mourinhoHali imeanza kuwa si shwari ndani ya kikosi cha Manchester United kutokana na Kocha Jose Mourinho kutokuwa na mwenendo mzuri na baadhi ya wachezaji.

Mourinho ameripotiwa mara nyingi kutokuwa na maelewano na kiungo Mfaransa, Paul Pogba na hii imetokana na kutomtumia mchezaji huyo kwenye mechi kama siku za mwanzo.

Mbali na Pogba, Luke Shaw, naye ameunga orodha hiyo baada ya kuonekana kutoelewana pia na Mourinho. Shaw alitupiwa lawama na Mourinho baada ya mchezo dhidi ya Brighton FC walioshinda kwa mabao 2-0 kwenye Kombe la FA akilalamikia kuhusu kiwango chake.

Kitendo hicho kimelifanya benchi la ufundi la timu hiyo na baadhi ya wachezaji kuanza kuona taswira mbovu ya timu hiyo siku za usoni kutokana na Kocha huyo kuingia kwenye matatizo na wachezaji hao wa United.

Tetesi zinaeleza kuwa, baada ya Pogba kutaka kuondoka klabuni hapo, Shaw naye anaelezwa kuihama timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika.

Saturday, 27 January 2018

MSANII WA BONGO FLAVER SHABIKI WAKUTUPWA WA YANGA AACHIA KICHUPA BAADA YA WANAJANGWANI HAO KUILAZA AZAM--JIONEE MWENYEWE


Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tz Bara Yanga leo wameilaza Azam 2-1 katika uwanja wa chamanzi Azam walikua wakwanza kujipatia goli kupitia kwa iddi dakika ya 3

yanga walisawazisha dk ya 30 kupitia kwa chirwa,kisha gadiel michae akaipatia timu yake ya yanga goli la ushindi kwa shuti kali.

bofya hapo chini kutizama kichupa cha msanii shabiki wa yanga alichokiachia baada ya wanajangwani hao kuwalaza wanalambalamba

https://www.youtube.com/watch?v=gkTNOK2I-ig

TAKWIMU ZAO KABLA YA LEO...
Zimekutana 31
Yanga shinda 12
Azam shinda 11
Sare 8

Yanga ilifunga mabao 41
Azam FC ilifunga mabao 40

Wednesday, 15 November 2017

JANGWANI MAMBO SAFI KUPITA NA INJINI YA MTIBWA




Kiungo mwenye kiwango cha kuvutia Mtibwa Sugar, Mohamed Issa ‘Banka’ ambaye anawindwa na Yanga amesema kuwa yupo mbioni kumaliza mkataba wake.

Kiungo huyo amesema kuwa baada ya mkataba huo yupo tayari kwa sasa kutua kwenye klabu yoyote itakayomhitaji.

Banka ambaye alitua Mtibwa Sugar mwaka jana anaweza kuchezea nafasi tano uwanjani ambazo ni sita, saba, nane, kumi na kumi na moja ambazo zote anazimudu vyema.

Kiungo huyo amekuwa akizitoa udenda timu kubwa za Simba na Yanga kutokana na umahiri wake wa kulisakata kabumbu, hivyo lolote linaweza kutokea usajili wa dirisha dogo.

Banka alisema kuwa, anatarajia kumaliza mkataba wake na klabu yake hiyo ya sasa licha ya kutotaka kuweka wazi anamaliza lini lakini amesema anaweza kutua kokote.

“Nakaribia kumaliza mkataba wangu na Mtibwa hivi karibuni ila siwezi kusema ni lini na sijajua kama nitaongeza ama nitabaki.


“Mimi ni mchezaji nipo tayari kwenda timu yeyote inayonihitaji ijapokuwa siwezi sema ni timu gani zimenifuata hadi sasa kwa kuwa sihitaji kuweka wazi kila kitu hadi kikamilike lakini ieleweke kuwa kuna timu zinanitaka na siyo moja,” alisema Banka.

SOURCE: CHAMPIONI

Thursday, 12 October 2017

NIOZIMA AFUNGUKA YA MOYON BAADA YA KUHAMIA MSIMBAZI ADAI BADO HAJARIDHIKA...............




Kiungo nyota wa Simba, Haruna Niyonzima amesema kiwango chake bado na hakijawa kama anavyotaka.

Niyonzima amezungumza na SALEHJEMBE na kusema kiwango chake hakijawa kama anavyotaka.

"Kweli sijafikia kama ninavyotaka, ndiyo maana nimeamua kufanya mazoezi ya ziada.

"Nafanya hivyo ili kuwa katika kiwango ninachotaka. Hii inatokana na kwamba sikupata muda mzuri wa mazoezi mwanzoni mwa msimu," alisema.

Niyonzima alichelewa kujiunga na kikosi cha Simba na alishindwa kujiunga nacho wakati kikiwa kambini nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya.

Wakati huo ndiyo alikuwa amejiunga na Simba akitokea Yanga lakini alibaki nchini kwao Rwanda kwa ruhusa ya uongozi wa Simba kwa kuwa alikuwa akisomea ukocha.

Tuesday, 10 October 2017

KENYETA AMJIA JUU ODINGA MUDA MFUPI BAADA YA KUBADILI GIA ANGANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA KENYA

Rais Uhuru Kenyatta amemjia juu Kiongozi wa NASA Raila Odinga baada ya kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini Kenya na kusema hata kama amejitoa Katiba ya Kenya haizuia uchaguzi kutofanyika

Kenyatta amesema kuwa Odinga alitaka uchaguzi urudiwe jambo ambalo limeigharimu nchi ya Kenya fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingeweza kutumika kujenga mahospitali na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi, lakini anashangaa mtu ambaye ametaka uchaguzi kurudiwa anajiengua tena.

"Rafiki yangu nasikia sasa umesema umejitoa baada ya kutupeleka peleka zaidi ya shilingi bilioni 12 hivi sasa zinatumika ili tufanye uchaguzi, pesa ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingetumika kujenga hospitali ya wananchi sasa zinatumika kwa uchaguzi ambao yeye ndiye aliitisha na sasa anasema hataki, kuna haki hapa jamanii, si mahakama ilisema IEBC haina makosa hayo masharti yote unatoa lakini tume hii si ndiyo imefanya viongozi hawa wengine wote kupatikana" alihoji Kenyatta

Mbali na hilo Kenyatta amesema kuwa wao wataendelea na mchakato wa uchaguzi kama kawaida na kusema huenda awepo au asiwepo Odinga uchaguzi utafanyika kama kawaida kama ambavyo tume ya uchaguzi ilitangaza.