Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Tuesday, 18 July 2017

VIDEO:TAZAMA HARMORAPA ALIVOTINGA MSIBANI KWA WAZIRI MWAKIEMBE


Msanii Hamorapa ameungana na Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, leo wameshiriki katika ibada ya kumuaga mke wa Dk Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe.

Pamoja na Mkapa, viongozi kadhaa wa Serikali akiwamo Jaji Kiongozi, Katibu Mkuu Kiongozi, mawaziri, wake wa viongozi wastaafu, wake wa mawaziri, wanasiasa na wasanii wameshiriki ibada iliyofanyika katika kanisa la KKT Kunduchi jijini Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya kuusafirisha mwili huo kuelekea mkoani Mbeya kwaajili ya mazishi. 

TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI
 
BONYEZA HAPA CHINI KUJIONEA MWENYEWE ALICHOKIONGELEA JERRY MURO SIKU CHACHE BAADA YA KUACHWA NA WAAJIRI WAKE WA ZAMANI YANGA



Monday, 10 July 2017

ROMA MKATOLIKI AFUNGUKA LIVE HAYA KUHUSU WALIOMTEKA

Mwanamuziki Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki” amesema kuwa tukio lililotokea miezi mitatu iliyopita lilikuwa na sababu nyingine zaidi ya muziki anaoufanya, tofauti na watu wanavyodhani.

Roma amesema katika mahojiano na EATV kwamba alijua kuwa atawakwaza baadhi ya watu kwa kutosema na kuweka wazi mambo kadhaa kuhusu tukio hilo ikiwemo kutekwa, walipopelekwa, kilichowatokea wakiwa huko walikopelekwa n.k lakini aliamua kutumia busara na kutosema kitu ili aweze kulinda sanaa na maisha yake kwa ujumla.

“Mimi najua nini kilipelekea wale jamaa kututeka. Ni zaidi ya muziki, japo chanzo ni muziki ndio maana walikuja kututeka tukiwa studio na si kanisani wala nyumbani. Unajua wananchi tayari walikuwa na video kichwani wakijua Roma anakuja kuongea hiki na kile, tunamaliza pale halafu usiku mwema.”

“Lile tukio lilikuwa linahitaji busara ili maisha yaweze kuendelea. Labda ningesema ukweli pengine ungekuwa ndio mwisho wa Roma kwenye muziki. Mashabiki wangeshangilia lakini kwa wadau mbalimbali mchango ndio ungekuwa umekwisha,” alisema.

Roma alisisitiza kuwa kama angeweka wazi jambo hilo siku ile ambayo alitoka, ingepelekeaa yeye kuacha muziki na kurudi Tanga kufanya mambo mengine, kwani hakuna mtu ambaye angetaka kuwa karibu naye tena.

“Toka nimetoka mpaka sasa sitaki kutazama video mbalimbali ambazo zinaonesha jinsi watu walivyokuwa wakihangaika kututafuta. Sitaki kutazama kwa sababu sitaki kukumbuka kabisa hali ambayo nilikuwa nayo kipindi kile. Pia sipendi kabisa kuona mtu mwingine yeyote anakwenda huko chimbo ambako tulikuwa tumewekwa tukipata mateso,” alisema.

Roma na wenzake walitekwa mwezi wa nne mwaka huu walipokuwa katika studio za kutayarisha muziki za Tongwe Records na kupelekwa kusikojulikana kwa muda wa siku tatu na kuja kuonekana wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini
USIACHE KUSOMA NA HABARI HII YA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI NA HALIMA MDEE KWA KUBONYEZA HAPA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI,ALLY HAPI AIBUKA KIVINGINE SAKATA LA HALIMA MDEE

Thursday, 8 June 2017

SASA MAMBO YAKO WAZI STEVE NYERERE AFUNGUKA ISHU YA SAUTI ZA MBOWE NA WEMA,MAJIBU HAYA HAPA




Mchekeshaji Steve Nyerere
Steve Nyerere
Steve kakanusha kuhusika na uigizaji wa sauti za mtongozo zilizovuma baina ya watu wanaodaiwa kuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mrembo Wema Sepetu wa Bongo Movie..

Kwanza mimi toka nimeanza kuigiza sauti sijawahi kuigiza sauti za viongozi wa chama fulani, Pili, kutongoza napo sio dhambi, ni sunna (akimaanisha ni jambo jema tu kwa mwanaume yoyote kulifanya). 
Tatu, sio kila kitu ambacho kimefanywa na familia fulani basi Steve anahusika. 

Limenikera na kuniumiza sana. Pia sio kwa Kingereza kile cha kubembeleza vile, nina uwezo huo? Na pia sio mimi peke yangu ninayeweza kuigiza sauti za watu, waigizaji wapo wengi.” alinukuliwa akisema Steve Nyerere.

Sunday, 4 June 2017

MSANII KUTOKA WCB AMPIGIA SALUTI ALIKIBA



Msanii mpya kutoka WCB, Lava Lava, amefunguka mambo mengi kuhusu muziki wake pamoja na kueleza jinsi anavyomkubali muimbaji Alikiba ambaye ni mpinzani mkubwa wa bosi wake, Diamond Platnumz.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo, Tuachane, amedai amekuwa akiufutilia muziki wa Alikiba kwa muda mrefu.

“Alikiba ni msanii mzuri sana, nampenda sana,” alisema Lava Lava. “Ni mkongwe kwenye muziki, miaka yote namuangalia na kujifunza vingi kutoka kwake”

Pia muimbaji hayo amedai haioni kama kuna bifu kati ya bosi yake na Alikiba ila anachokiona ni ushindani kati ya wawili hao.

“Mimi naona baada ya ushindani kuanzishwa na muziki wetu umefika mbali, kwa hiyo kushindanishwa kwao mimi naona ni sawa kwa sababu muziki unafika mbali na watu wanakuwa na speed ya kazi lakini siyo kwa ubaya,” alisema Lava Lava.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amedai alikaa kipindi cha mwaka mmoja WCB bila kuona na Diamond

GIGY AUMBUKA AYALA MATAPISHI YAKE MWENYEWE



IKIWA imepita miezi michache tangu ajiapize kuwa hatakuja kujichora tattoo ya mwanaume yeyote atakayekuwa naye katika uhusiano, muuza sura kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameumbuka baada kunaswa akiwa amejichora jina la mwandani wake, Mourad Alpha ‘Moj’.
Mwanadada huyo ambaye mara kwa mara amekuwa akiingia kwenye mgogoro na Moj kwa madai kuwa amekuwa akimpiga bila sababu za msingi hivyo anatumia nguvu kubwa kuachana naye lakini anashindwa, amejikuta akiumbuka kwa kujichora tattoo ya jina lake. Alipobanwa baada ya kunaswa na tattoo hizo, Gigy alisema; “Haa unaniuliza, sijui hata nikujibu nini? Nguvu ya mapenzi ndiyo imenisababisha kufanya hivi, migogoro ni kawaida katika mapenzi na kupigwa kila wakati nimeshazoea

Thursday, 4 May 2017

NAY WA MITEGO KUACHIA REMIX YA WAPO KWAAJILI YA RAIS MAGUFULI


Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo ‘Wapo’ kwaajili ya  Rais John Pombe Magufuli iko tayari na inaweza kuachiwa muda wowote.
Rais Magufuli  aliufungulia ‘original version’ ya wimbo huo baada ya kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili na kumtaka rapa, Nay wa Mitego kuongeza baadhi ya maneno katika wimbo huo ili uwaguse watu wengi zaidi.
Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo huo iko tayari na ameongeza vitu ngingi ndani ya wimbo huo.
“Kusema kweli wimbo wa Mh Rais umekamilika na muda wowote unaweza kutoka,” alisema Nay. “Nimeongeza mambo mengi ndani yake, kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili ya moto mwingine kwa sababu bado ‘Wopo’ yenyewe inaendelea kufanya vizuri,”
Rapa huyo amedai hawezi kusema ni lini project hiyo itatoka.
Katika hatua nyingine rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kumuunga mkono katika muziki wake pamoja na kujitokeza kwa wingi katika tour yake ya  ‘Wapo’ ambayo imeingia ndani ya jiji la Dar es salaam